Ibuka yafungua kiwanda cha alizeti

06Dec 2017
Neema Sawaka
Nipashe
Ibuka yafungua kiwanda cha alizeti

CHAMA  cha  Ushirika cha Ibuka, Multipurpose  Cooperative Society Ltd., kilichopo Msalala  wilayani Kahama,  kimefungua kiwanda  cha kukamua alizeti na kugawa mbegu tani tano kwa wananchi  4,772.

Meneja wa chama  hicho, Mkama Msiba,  alisema wameamua kufungua kiwanda hicho kusaidia jamii inayoishi katika vijiji  14  vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ili iachane na dhana ya kutegemea ajira kutoka migodini.   

Alisema wameamua kuwawezesha wanachama hao ili waweze kujikwamua kiuchumi na alizeti hiyo ikilimwa na kuvunwa  itanunuliwa na ushirika huo.

Mwenyekiti wa Ibuka, Raphael Buhulula alisema kiwanda hicho kimegharimu Sh. milioni  90 na  mwaka jana walilima  na kupata  magunia  208 ambayo yatatumika  kama  malighafi ya kuanzia kwenye kiwanda hicho.