Infinix yaipamba siku ya Valentine kwa uzinduzi wa duka la pili Dar

14Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR
Nipashe
Infinix yaipamba siku ya Valentine kwa uzinduzi wa duka la pili Dar

Katika kusheherekea sikukuu ya wapendanao (Valentine's), kampuni ya simu, Infinix Mobile Tanzania imezindua rasmi duka Jipya, maarufu kama Infinix Smart Hub, lililopo kwenye jengo la China Plaza Kariakoo kwa lengo la kuwafikia wateja wengi.

Katika uzinduzi huo Afisa wa Mahusiano wa Kampuni hiyo, Aisha Karupa, amesema Infinix imejipanga katika kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake maeneo mbalimbali na kuondoa hofu kwa wateja hao ya kuwafikia kwa uharaka na katika kutekeleza hilo Infinix Smart Hub litakuwa linatoa huduma kwa siku saba za kila wiki kuanzia  jumatatu hadi jumapili kuanzia saa 9:00 asubuhi hadi saa 11:30 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi huo, Karupa ametoa shukrani za dhati kwa Watanzania kupokea bidhaa zao zilizo bora na zenye uhakika kwa matumizi.

“Kwa mapenzi yenu tutaendelea kutanua wigo ili kuhakikisha mnapata huduma stahiki kama vile simu na bidhaa nyingine za Infinix zenye ubora zaidi zikiwa chini ya 'Warranty' ya mwaka mmoja na mwezi moja pamoja na elimu ya bure kuhusiana na utunzaji na utumiaji wa simu za Infinix kwa muda mrefu pasipo kuwaletea shida ya aina yoyote” amesema Karupa.

Naye Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo, Saiphone Asajile ameeleza mafanikio waliyoyapata kwenye mauzo ya Infinix tangu kuingia kwake rasmi Tanzania mwaka 2018 na Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka Infinix hasa kwa kipindi hiki cha Valentine.

“Watanzania wameonyesha upendo wa hali ya juu sana kwetu na hadi kufikia hatua ya kuzindua duka la pili la kisasa sio hatua ndogo, kwani kuna kampuni nyingi za simu tumezikuta lakini hawajafanikiwa kufanya hili tunalolifanya Infinix, hiki ni kiashirio tosha Infinix imeliteka soko la simu kwa asilimia kubwa lakini vile vile katika kuendeleza upendo kama ilivyo kawaida yetu katika Msimu huu wa Valentine Infinix inakupa ofa ya 10%, Infinix gift package na chakula cha usiku kwa wewe na umpendaye katika Mgahawa wa kisasa” amesema Asajile

Habari Kubwa