Jafo aagiza kukamatwa kwa aliyetelekeza makontena ya uchafu bandarini

03May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Jafo aagiza kukamatwa kwa aliyetelekeza makontena ya uchafu bandarini

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo, ameagiza kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Seif for Tobacco Trading Co. Ltd anayefahamika kama Kaissy, baada ya kuingiza makontena zaidi ya 500 yenye Molasesi na kuyatekeleza hadi kuharibika katika bandari ya Dar.  

Waziri Jafo amesema Tanzania haiwezi kugeuzwa kuwa dampo kwa kuruhusu bidhaa kutoka nje ya Nchi ambazo muda wake wa matumizi umeisha kuingizwa kwa lengo la kutupwa kiholela.Imebainika kuwa mfanyabiashara huyo aliingia nchini kwa hati ya utembezi (tourist) na baadaye kupatiwa kibali cha uwekezaji kupitia Export Processing Zone (EPZA) kilichomruhusu kuwekeza katika uzalishaji wa shisha, kibali ambacho kilifutwa baada ya kugundulika kuna udanganyifu.Aidha, Waziri Jafo amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC kufanya ukaguzi katika bandari kavu zote nchini ili kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini zikiwa zimeisha muda wake wa matumizi na kutelekezwa.

Habari Kubwa