JKT Mlale yajikita kilimo cha mahindi kukidhi mahitaji chakula

20Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
SONGEA
Nipashe
JKT Mlale yajikita kilimo cha mahindi kukidhi mahitaji chakula

KATIBU wa Kamati ya Kilimo Mkakati, Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Luteni Kanali  Peter Lushika, amesema kikosi cha 842 Mlale kilichopo Songea mkoani Ruvuma kimejikita katika kilimo cha mahindi ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya chakula ya jeshi hilo na nje ya jeshi.

KATIBU wa Kamati ya Kilimo Mkakati, Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Luteni Kanali  Peter Lushika.

Luteni Kanali Lushika,  amesema mwaka huu wamelima Ekari 1,000 lakini wamejipanga kuhakikisha wanaongeza idadi ya Ekari za mahindi katika kikosi hicho lengo ikiwa ni kutekeleza agizo la kujitegemea katika suala zima la chakula.

Naye Kaimu Kamanda wa kikosi 842 JKT Mlale, Meja Godwin Mapunda amesema ukiacha shamba la mahindi walilolima pia wanakiwanda cha kuchakata mahindi kikosi hapo. 

Meja Mapunda amesema kiwanda hicho kinasaidia kuchakata mahindi pale yanapokuwa yamevunwa kwa ajili ya kupata unga ambao unatumiwa kwa matumizi ya chakula.

Habari Kubwa