Kairuki aonya walimu ukiukwaji maadili

18Mar 2023
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Kairuki aonya walimu ukiukwaji maadili

(TAMISEMI), Angellah Kairuki, amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali walimu watakaobainika kwenda kinyume na maadili ya kazi.

Waziri Kairuki aliyasema hayo juzi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) uliofanyika jijini Dodoma uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa kielektronikiunaojulikana kama ‘Teachers Service commission System (TSCMIS)’.Alisema TSC ina wajibu wa kuwasimamia walimu ili watimize majukumu yao na kwamba walimu wanaitegemea tume hiyo, hivyo inapaswa kufanya kazikwa weledi ili kuhakikisha walimu wanapata haki zao za msingi katikautendaji kazi wao wa kila siku.

“Serikali haitakuwa tayari kuwavumilia walimu ambao wataenda kinyumecha maadili ya kazi. Nasisitiza  TSC simamieni walimu kuhakikishawanafanya kazi katika mazingira bora,” alisema.

 

 Kairuki pia aliagiza walimu kuhakikisha wanasimamiauendelezaji mradi wa kuboresha elimu ya sekondari nchini (SEQUIP) naule wa Boost wa kuboresha elimu ya awali na msingi.

 

Alisemakatika mradi wa SEQUIP serikali imeridhia kutumia Sh. trilioni 1.2 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari 1026.

“Mradi wa BOOST serikali imeridhia kutumia Sh. trilioni 1.15 katika kipindi chamiaka mitano kwenye mwaka wa fedha 2022/23 zitumike kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu na suala zima la miundombinu ikiwamo kuhakikisha mazingira ya ujifunzaji na kufundishia yanakuwa mazuri,” alisema.

Alisema kupitia mradi wa BOOST, serikali itaendelea kuhakikishawalimu wanafundishwa kuzingatia ujuzi, lakini pia waendelee kuboresha mitaala na walimu ili kuendana na wakati ikiwemokuhakikisha wanakuwa na uendelevu wa kuwapatia walimu mafunzo kazini.

 

Kuhusu mfumo wa TSCMIS, aliwataka TSC kutumia mfumo huo vizuri ilikurahisisha utatuzi wa kero mbalimbali za walimu, ikiwemo kupatataarifa sahihi za walimu.

Katibu wa TSC, Paulina Nkwama, aliishukuru serikalikutokana na kuajiri walimu,kupandisha madaraja walimu, vyeo, pamoja nakulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara.

 

 

Habari Kubwa