KCB yatoa elimu kodi kwa wafanyabiashara

03Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
Mwanza
Nipashe
KCB yatoa elimu kodi kwa wafanyabiashara

WAFANYABIASHARA wadogo na wakubwa wamenufaika tena na elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, kupitia kongamano kubwa lililoendeshwa na Benki ya KCB jijini Mwanza wiki iliyopita.

Hilo ni kongamano la pili kuendeshwa na benki hiyo, baada ya mapema mwaka huu kufanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara 200, huku wakinufaika na kubadilishana mawazo kutoka kwa wafanyabiashara wa nje ya nchi.

 

Kongamano hilo lilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa

na changamoto mbalimbali za kibiashara zikiwamo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika masuala ya kodi na nyinginezo.

Nia kubwa ya Benki ya KCB ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

 

Meneja wa Tawi la KCB Benki Mwanza, Emmanuel Mzava, aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa

kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika

kukabiliana na changamoto za kibiashara.

 

Alisema tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea

kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika sekta ya SME kwa

kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli

zao za kibiashara.

 

Mzava alisema mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safari mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao, ambapo utasababisha wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao na kwamba Benki ya KCB inatambua umuhimu wa wafanyabiashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi, lakini inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanyabiashara hao

hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

 

 

Swetbert Thomas, mtaalamu wa masuala ya kodi, aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu umuhimu wa kuelewa

mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara zao.

 

 

 

Habari Kubwa