Madalali Bahi wavamia ufuta

26Feb 2016
Leonce Zimbandu
Dar
Nipashe
Madalali Bahi wavamia ufuta

WAKULIMA wa zao la ufuta katika Wilaya Bahi mkoani Dodoma, wamesema hawanufaiki na biashara ya zao hilo baada ya madalali kuvamia na kushusha bei kwa maslahi yao binafsi.

Zao la Ufuta.

Malalamiko hayo yametolewa ili kuiomba serikali kuingilia kati mgogoro upangaji bei kiholela baada ya kukosekana kwa bei elekezi ya zao hilo.

Mkulima wa ufuta, Joel Ndalu, mkazi wa Wilaya ya Bahi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Nipashe mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.

Alisema kisheria madalali hawana mamlaka ya kupanga bei, lakini kutokana na usimamizi mdogo wa sheria, hivyo kikundi cha watu wachache huamua kujichukulia sheria ya kupanga bei.

"Zao la ufuta ni miongoni mwa mazao ya kibiashara, hivyo serikali inapaswa kuweka kipaumbele kwa kuhakikisha inadhibiti uzalishaji na kuwa na bei ya uhakika katika soko," alisema.

Habari Kubwa