Magereza waanza kujenga kiwanda cha ngozi

12Jan 2019
Mary Mosha
Moshi
Nipashe
Magereza waanza kujenga kiwanda cha ngozi

UWEKEZAJI wa kiwanda kipya cha kutengeneza viatu kinachojengwa unatarajia kutoa ajira za kudumu kwa Watanzania 3,000 kitakapokamilika.

Naibu Mkrugenzi wa kiwanda hicho kitakachoitwa Karanga Leather Industries Co.Ltd, Shalua Magandi amesema wafanyakazi ambao watakuwa siyo wa kudumu watafikia watu 4,000 ifikapo mwaka 2020.

Alisema ujenzi huo unatarajiwa kuanza rasmi Januari 15 mwaka huu na utakamilika katika kipindi cha miezi 16 ukiwa umegharimu zaidi ya Sh. Bilion 67.

Magandi alikuwa akitoa taarifa jana kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati alipotembelea kiwanda hicho.

Alisema mbali na ujenzi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni lakini walishapata mashine mpya na za kisasa ambazo zimesaidia kukuza uzalishaji kutoka jozi 150 kwa siku hadi jozi 400 kwa siku.

“Ujenzi wa kiwanda unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo kwani mikataba yote imeshapelekwa kwa mwanasheria mkuu kwa ajili ya hatua za mwisho na tunatarajia mapema Januari 15 ujenzi utaanza na kukamlika ndani ya miezi 16,”alisema.

Aidha Waziri Mwagama aliwataka kuendeleza jitiada za kuhakikisha mradi huo unatekelezeka kwa wakati na kuwa sehemu ya kuwasaidia wananchi.

“Huduma mnazotoa ni za hali ya juu lakini kinachosikitisha ni kwamba watu hawafahamu mnafanya nini licha ya ubora wa bidhaa zenu, jitangazeni ili watu wafahamu mnavyofanya ili muweze kufanya biashara na kuingiza mapato,”alisema

Alisema pia kwa sasa wazeni kuzalisha kwa kiwango kikubwa ili muweze kuingia kwenye soko la la Afrika Mashariki na la dunia kwa ujumla lengo likiwa ni kupata fedha za kigeni kwa maendeleo ya Taifa letu.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Moshi, akiwamo Agapity Macha alisema uwepo wa kiwanda hicho kinaweza kukuza uchumi wa mtu moja moja pamoja na wa mkoa.

Alisema mbali na kukuza uchumi kutatoa ajira za moja kwa moja wa wanataluma na wasio na taaluma zaidi ya 9,000 hii ni ongezeko kubwa la ajira kwa vijana.

Nancy Moses aliishauri serika kuhakikisha inaongeza jitihada za kujitangaza ikiwa ni pamoja na kutembea katika mashule, na kuwapunguzia bei wafanyabiashara wadogo watakaoweza kuzungusha ndani na nje ya nchi .

“Tunashauri watendaji wa kiwanda hicho kuunguza urasimu wa utoaji wa taarifa pamoja na kujikita katika kukitangaza kiwanda hicho kupitia vyombo vya habari ..

Habari Kubwa