Magonjwa ya mlipuko changamoto inayowakabili wanawake wafugaji

03May 2021
Zanura Mollel
ARUSHA
Nipashe
Magonjwa ya mlipuko changamoto inayowakabili wanawake wafugaji

Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC) mkoani Arusha kupitia Mradi wa Mabadiliko ya tabia nchi unaoendeshwa mkoani humo limekutana na viongozi wa Halmashauri ya Longido na wadau kutoka Tarafa ya Kitumbeine kujadili na kuweka mipango mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa tarafa hiyo.

Mratibu wa mradi tabia nchi, Grace Sikorei.

Mratibu wa mradi huo, Grace Sikorei amesema halmashauri hiyo imepokea mapendekezo mbalimbali ya baraza hilo na kuahidi kufanyia kazi, na kusema kuwa; "Tulibaini kuna uhaba wa maji,upungufu wa nyanda za malisho,uhaba wa chakula cha kutosha,kuongezeka kwa magonjwa ya milipuko kwa binadamu na mifugo pamoja na miundombinu " amesema Sikorei.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dk. Juma Mhina, amesema kwa sasa bajeti ya serikali imeshafungwa, lakini wakitokea wadau mbalimbali wa maendeleo watatumia nafasi hiyo kama fursa ya kutatua changamoto hizo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Simon Oitesoi, amesema bajeti ijayo watajitahidi kuingiza miradi hiyo kwenye bajeti, huku akilitaka shirika hilo kuendelea kusaidia miradi ambayo ipo ndani ya uwezo wao pamoja na kuwatafutia wadau.

 

Habari Kubwa