Mbinu kilimo zaleta manufaa

12Jun 2017
Beatrice Philemon
Nipashe
Mbinu kilimo zaleta manufaa

WAKULIMA 404 katika wilaya za Kilosa na Gairo mkoani Morogoro, wataanza kunufaika na mazao wanayolima, baada ya Ushirika wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sugeco)-

kuwafundisha mbinu bora za kilimo ili kuzalisha vyakula yenye virutubishi vingi lengo likiwa kuboresha lishe na kuongeza kipato kwa ngazi ya kaya.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa mradi wa kuboresha lishe na kuongeza kipato ngazi ya kaya, Joseph Masimba, mara baada ya kufanya ziara katika vijiji vya Zombo, Nyameni, Ulaya-kibaoni, Kisanga, Msolwa, Magubike, Kiegeya, Mtumbatu, Ngiloli na Ibuti kuona kitu gani kimeshafanyika tangu wakulima wapewe mafunzo na Sugeco mwaka 2016 .

“Kabla ya kujikita katika kilimo cha mahindi lishe, Sugeco ilitoa mafunzo kwa wakulima na baada ya mafunzo kila mkulima alipewa kilo 2.5 ya mbegu ya mahindi lishe ili kwenda kupanda katika robo eka ya shamba lake,” alisema.

Mafunzo hayo yalitolewa na Sugeco mwaka 2016 katika vijiji 10 vilivyopo kwenye mradi na baadhi ya wakulima wameanza kuvuna mahindi lishe na uzalishaji umeongezeka kutoka kwenye robo eka kwa kuvuna magunia 6-7.