Mbunge awalilia wachimbaji wadogo Shinyanga

07Mar 2017
Mohab Dominick
KAHAMA
Nipashe
Mbunge awalilia wachimbaji wadogo Shinyanga

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Salome Makamba, ameishauri serikali kuwanusuru na hali mbaya ya mazingira wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo, mkoani hapa.

Makamba alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na wachimbaji hao baada ya kufanya ziara katika maeneo yao ya uchimbaji na kubaini kasoro nyingi katika shughuli za uchimbaji.

“Katika ziara hii nimebaini vitu vingi vinavyopaswa kushughulikiwa na serikali, kwanza serikali yenyewe imewaruhusu wachimbaji kuendelea kuchimba madini hapa Nyaligongo bila kuangalia mazingira yakoje, pili wako hatarini kufukiwa na vifusi kwa uchimbaji mbovu,” alisema.

Aidha, alisema licha ya uchimbaji mbovu unaoendelea katika eneo hilo kutokana na kutumia dhana duni, wanahatarisha maisha yao kila kukicha kutokana na ruhusa waliyopewa na Rais, idadi ya wachimbaji inazidi kuongezeka kutoka asilimia tano hadi asilimia nane.

Habari Kubwa