Kutoakana na msako ambao umekuwa ukifanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa Njombe hatimaye mwendelezo wa kukamata watu wenye nia ovu ya kuchakachua pembejeo za mbolea na kuwatia hasara wakulima kwa mara nyingine sasa shehena ya mifuko 776 iliyo jazwa mchanga imekamatwa tayari kwa kuwauzia wananchi.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka, amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapo baini kuuziwa mbolea wanazotilia mashaka huku Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Deo Sanga, akimtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha wahusika wote wanashughulikiwa ipasavyo.
Kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Njombe Mjini Deo Mwanyika ameiomba serikali kushughulika na wale wote walio husika na uhalifu huo wenye lengo la kuwatia hasara wakulima huku akiomba serikali kuwafidia wakulima walipata hasara baada ya kununua mbolea feki.
Kutoakana na hali hiyo iliyo jitokeza waziri wa kilimo husei bashe amemuagiza mkuu mkoa wa Njombe Antony Mtaka kumata Mshindo Msola ambaye ni Meneja Mauzo wa Kampuni Ya Minjingu na viongozi wa nfra ili kubaini madudu hayo.