Mkakati korosho washika kasi

27Mar 2018
Margaret Malisa
Pwani
Nipashe
Mkakati korosho washika kasi

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amezindua upandaji wa mikorosho mipya katika shamba la Ruvu JKT lililoko Mlandizi Wilaya ya Kibaha.

korosho.

Uzinduzi wa upandaji wa mikorosho mipya una lenga kuonyesha umuhimu wa zao hilo kwa mkoa wa Pwani, baada ya serikali kulitambua zao hilo kuwa ni moja ya mazao ya biashara ya kimkakati nchini sambamba na mazao ya pamba, kahawa, tumbaku na chai.

 

Ndikilo aliwataka wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo, ili liweze kuwainua kiuchumi na kuwa serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imetoa kilo 7,182 za mbegu bora za korosho kwa mkoa wa Pwani na kusambaza katika halmashauri zote. 

 

Alisema mbegu hizo zinakadiriwa kuzalisha miche bora 1,039,687 ya korosho ambayo tayari imeanza kutolewa bure kwa wakulima.

 

Alisema miche inayotokana na mbegu hizo inaanza kuzaa korosho miaka mitatu baada ya kipandikizwa ambapo mavuno yanaongezeka kadri matawi ya mmea yanavyoongezeka na kusambaa.

 

“Utafiti unaonyesha mmoja wa korosho za aina hii unatoa wastani wa kilo 40 za korosho kwa msimu na ekari moja miti  28 ya korosho kwa nafasi  ya mita 12 kati ya mti na mita 12 kati ya mstari hadi mstari, pia ina uwezo wa kuzalisha wastani wa kilo 1,200 kwa msimu, kwa hiyo upandaji wa miche hii utaleta tija kubwa katika uzalishaji wa korosho mkoani hapa,” alisema.

 

Alisema ugawaji wa miche ya korosho bure, unaonyesha jitihada za serikali imayolenga kuwakomboa wananchi kiuchumi, hivyo aliwataka viongozi wa halmashauri kuunga mkono jitihada hizo za serikali kwa kuhakikisha wakulima watakaopata miche hiyo bure wanaipanda na kuitunza.

 

 

 

 

Habari Kubwa