Mkazi wa Njombe akabidhiwa gari lake la ‘Kapu la Wana’

13Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mkazi wa Njombe akabidhiwa gari lake la ‘Kapu la Wana’

Mkazi wa Njombe Rehema Lawrence Mbuya, amekabidhiwa gari aina ya Suzuki Carry lenye thamani ya shilingi milioni 10 baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya "Kapu la Wana" inayoendeshwa na bia ya Plisner Lager.

Gari aina ya Suzuki Carry ambayo amezawadiwa mshindi wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’ inayoendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Pilsner Lager.

Rehema ni mshindi wa tatu kupatikana tangu promosheni hiyo kuanza baada ya Privatus Mujuni wa Mubela Kagera ambaye alijishindia Power tiller na Jackline Minja aliyejishindia vifaa vya studio ya picha.

Kupitia kampeni ya ‘Kapu la Wana’, bia ya Pilsner imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo zitatolewa kwa washindi watano ambapo kila mmoja atajishindia vifaa kwa ajili ya kukuza biashara yake vyenye thamani ya shilingi milioni 10.

Rehema amekabidhiwa gari la kubeba mizigo aina ya Carry kwa ajili kumsaidia kupeleka mizigo ya wateja wake.

Wakazi wa Njombe wakifurahia bia yao pendwa aina ya Pilsner Lager muda mfupi kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry mshindi wa kampeni ya ‘Kapu la Wana’ inayoendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Pilsner Lager.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi hao, meneja chapa wa SBL Ester Raphael alisema zawadi zilizotolewa ni muendelezo wa kampeni hiyo inayolenga kuwawezesha vijana wajasiriamali wapambanaji kufikia malengo yao kupitia Bia ya Pilsner.

“Pilsner, bia ya wapambanaji, leo inawazawadia wapambanaji wawili vifaa kwa ajili ya kukuza biashara zao. Siku chache zilizopita, tulishuhudia mpambanaji mwingine Privatus Mujuni kutoka Muleba Mkoani kagera naye akiwezeshwa pia. Kampeni bado inaendelea na kila mpambanaji ana nafasi ya kushinda, tuendelee kushiriki,” alisema Ester

Kwa upande wake Rehema alisema changamoto kubwa aliyokuwa anakabiliana nayo ni ukosefu wa usafiri wa kufikisha mizigo kwa wateja na kusema gari alilopewa litamsaidai kuimarisha biashara yake na kumfanya asonge mbele kwa haraka zaidi.

“Nina kila sababu ya kuishukuru bia ya Plisner kuputia kampeni ya ‘Kapu la Wana’ kwa uwezeshaji huu mkubwa kwangu. Gari hili litanifanya niweze kuwahudumia wateja wangu vizuri zaidi kwa kuwafikishia mizigo,” alisema

Katibu tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George akimkabidhi mshindi wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’ Rehema Lawrence Mbuya mfano wa funguo ya gari baada ya kuibuka mshindi katika promosheni hiyo.

Kwa mujibu wa Ester, shindano hilo ni mahususi kwa ajili ya vijana wapambanaji wanaofanya shughuli mbalimbali kama ukulima, uvuvi, vinyozi n.k. ambao wanatamani kufikia malengo makubwa lakini wanapata changamoto katika upambanaji wao kutokana na kukosa uwezeshwaji hali inayowapungizia kasi ya kufikia malengo yao na mafanikio kwa wakati.

“Pilsner ni bia ya vijana wapambanaji, wasiokata tamaa na wenye kiu ya kufikia mafanikio makubwa.Tumeona ni vyema kuwawezesha wateja wetu wenye kiu ya mafanikio kwa kuwapa vitendea kazi ili wazidi kusonga mbele zaidi.”

Alifafanua kuwa moja ya vigezo vitakavyotumika kupata washindi ni pamoja na umri usiozidi miaka 35 mshiriki atahitajika kuwa na biashara isiyozidi miaka miwili pamoja na kuwa na stori ya kuvutia juu ya namna alivyoanza na wapi anataka kuipeleka biashara hiyo.

Habari Kubwa