Mkazi wa Songea ajishindia bodaboda ya NMB MastaBata Kotekote

20Nov 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Mkazi wa Songea ajishindia bodaboda ya NMB MastaBata Kotekote
  • Wengine 75 wazoa zaidi ya milioni 7

Benki ya NMB imepata mshindi wa pili wa bodaboda, Charles Mbwilo kutoka Songea mkoani Ruvuma kupitia droo ya  shindano la NMB  MastaBata Kote-kote.

Mshindi wa kwanza wa Bodaboda katika Kampeni ya Mastabata – Kotekote ya Benki ya NMB, Asumwisye Mwajeka (wapili Kushoto) akiijaribu pikipiki baada ya kukabidhiwa katika benki ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa.

Kushoto ni Meneja mwandamizi wa Idara ya Biashara za Kadi, Manfredy Kayala, kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mkwawa, Happiness Pimma na wapili kulia ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu, Manyilizu Masanja.

Katika kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh. milioni 350 zitatolewa kwa washindi 854 ikiwa ni pamoja na zawadi za pikipiki na safari ya Dubai kwa washindi saba pamoja na wenza wao. Akizindua droo ya pili ya mchezo huo katika Tawi la NMB - Mkwawa, mkoani Iringa,  Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Manyilizu Masanja alisema lengo kubwa ni kuhamasisha matumizi ya NMB mastercard na Lipa Mkononi(mastercard QR) kwa wateja wake. Masanja alisema wateja wakifanya miamala yao kupitia kadi ya NMB mastercard au Lipa  Mkononi (mastercard QR) au mtandaoni watakuwa wamejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya ushindi katika droo zijazo. Naye, Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi,  Manfred Kayala aliwahimiza wateja kuendelea kutumia njia hiyo kufanya miamala ili waingie kwenye droo hiyo na baadae kushinda. Kwa upande wake mshindi wa bodaboda wa wiki iliyopita, Asumwisye Mwajeka baada ya kukabidhiwa zawadi yake alisema;

 "Niwahamasishe vijana wenzangu msitembee na pesa mikononi au mifukoni, faida yake mimi nimeiona. Nimefurahi kupata bodaboda," alisema.

Tayari Sh. milioni 15 zimetolewa kwa washindi 150 mpaka sasa na bodaboda mbili zikiwa na thamani ya Sh. milioni 6.

Habari Kubwa