Mkenda asisitiza matumizi mbegu bora

25Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Moshi
Nipashe
Mkenda asisitiza matumizi mbegu bora

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, ameipongeza Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu TOSCI, kwa kazi nzuri, iliyopelekea Banda la TOSCI, kushinda tuzo ya banda bora.

Amewasisitiza wakulima wote wa Tanzania, kutumia mbegu zenye alama ya TOSCI ambazo ndizo mbegu zilizothibitishwa kutumika nchini.
 
Waziri Mkenda, alizitoa pongezi hizo katika mahojiano, baada  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, zilifanyika kwenye viwanja vya Pasua, nje kidogo ya mji wa Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 
Waziri Prof. Mkenda alisema TOSCI imefanya kazi nzuri ya kurahisisha uhakiki wa mbegu kwa wakulima kwa kutumia njia za kisasa za kielektroniki, kuhakiki mbegu, kwa kutumia simu ya mkono, hivyo kuliwezesha Taifa kutumia mbegu zenye ubora uliothibitishwa na TOSCI, na pia kuisifu TOSCI kuyatumie maonyesho hayo kutoa elimu kwa umma, sio tuu kwa wananchi waliofika viwanjani, bali pia banda la TOSCI, limetoa elimu kubwa kupitia vipindi vya redio na TV vya Banda la TOSCI.
 
Prof. Mkenda alisema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imepania kufanya mapinduzi ya kweli ya kilimo, na kutoa umuhimu wa pekee kwa utafiti, ambapo bajeti ya utafiti imeongezwa maradufu, ambapo kwa kuanzia, itatumia sehemu ya Sh. bilioni 8 zilizotolewa na IFAD kwa serikali ya Tanzania, kwa kuzielekeza kwenye utafiti.
 
Akizungumzia umuhimu wa utafiti, Prof. Mkenda alisema: “ Naamini huko tunakowenda, utafiti ni suala muhimu sana kwenye kilimo kuliko ambavyo tumeweza kuamini huko zamani, ili tuweze kuendana na mbadiliko ya tabianchi, tuweze kuendana na mazingira yetu, ili kuendana na aina ya udogo, na afya ya udongo tunaotumia, lazima tufanye utafiti.”

Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngediagi, alisema ushindi ni faraja kwa TOSCI nzima, menejimenti na wafanyakazi wote wa TOSCI ambao wanajituma kwa bidii na unazidi kuwapa ari ya kuendelea kujituma, kuwatumikia Watanzania.
 
 

Habari Kubwa