Momba yapiga `stop' vipimo visivyo rasmi ununuzi mazao

21Apr 2016
Bosco Nyambege
Momba
Nipashe
Momba yapiga `stop' vipimo visivyo rasmi ununuzi mazao

HALMASHAURI ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe imepiga marufuku wafanyabiashara kutumia vipimo visivyo rasmi wakati wa kununua mazao kwa wakulima.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Methew Chikoti, alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namsinde kata ya Mkulwe wilayani hapa mwishoni mwa wiki.

Alisema kumekuwa na kasumba ya wafanyabiashara kutumia vipimo ambavyo si rasmi, jambo husababisha mkulima kunyonywa.

“Unakuta baadhi ya wafanya biashara kununua mazao kutoka kwa wananchi hao kwa kutumia ndoo aina ya Mozambiki ambayo ni kubwa ukilinganisha na ndoo aina ya mboni ambayo inakubalika kuwa na vipimo halisi,” alisema Chikoti.

Habari Kubwa