Mradi wa maji wa bil. 1.8/- wasainiwa

13May 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mradi wa maji wa bil. 1.8/- wasainiwa

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (Mwauwasa), imesaini mkataba na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors Ltd ya mkoani Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo,-

wilayani Busega mkoani Simiyu utakaonufaisha wananchi wapatao 12,000 wa vitongoji vya Bukabile, Bulima na Mwagulanja.

Hafla ya utiaji saini ilifanyikia Mei 10, 2019 wilayani Busega na kushuhudiwa na wananchi, watendaji wa serikali na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ambaye alisema zaidi ya asilimia 74 ya wananchi wa Busega watakua na uhakika wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Mhandisi Anthony Sanga, akielezea utekelezaji wa mradi huo alisema ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, baada ya ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa Nyashimo ya kuwapelekea majisafi na salama.

“Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli alivyopita hapa Nyashimo wakati wa ziara zake aliwaahidi wananchi wa hapa kuwatatulia kero ya maji na aliiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha inatekeleza mradi haraka iwezekanavyo,” alisema Mhandisi Sanga.

Alisema mradi utatekelezwa kwa miezi 15 na utagharimu Sh. bilioni 1.8 na unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Aliongeza kuwa utekelezwaji wa mradi ni neema kwa wananchi wa Busega na aliwasihi kuchangamkia fursa zitokanazo na ujenzi wake kuanzia hatua za awali za utekelezaji na alimuagiza Mkandarasi kuhakikisha anatekeleza mradi kwa ufanisi mkubwa na kutoa kipaumbele kwa jamii inayozunguka kuwa ya kwanza kunufaika.

ayokabidhiwa kwa niaba ya Wizara ya Maji na alimsisitiza aendelee na moyo huo wa kizalendo na aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi na wafanyakazi wa Mwauwasa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu, Dk. Raphael Chegeni, aliyekuwa miongoni mwa viongozi walioshuhudia tukio hilo, alisema kero kubwa waliyokuwa nayo wananchi wa jimbo lake ni ukosefu wa majisafi na salama na tayari mwarobaini wake umepatikana.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkandarasi, Sabato Boas aliahidi kutekeleza mradi kwa muda mfupi kadiri itavyowezekana na kwa utaalam unaotakiwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Habari Kubwa