Nguhulla: Nitaendelea kumshauri Magufuli masuala ya meli

05Sep 2019
Mary Geofrey
Dar es Salaam
Nipashe
Nguhulla: Nitaendelea kumshauri Magufuli masuala ya meli

MBOBEZI wa Kimataifa katika shughuli za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli (FICS) Julius Nguhulla amesema  ataendelea kumshauri, Rais John Magufuli kuhusu sekta ya meli nchini kwa maslahi ya Watanzania wote.

Julius Nguhulla.

Nguhulla amesema Juni 3 mwaka huu, kwa nia njema alimuandikia barua ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Meli Tanzania (Tasac).

Nguhulla ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo ni kuisaidia sekta ya usafiri wa meli katika kukuza uchumi wa taifa.

Amesema katika barua hiyo, alimuomba Rais Magufuli kuishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu wa tozo utoaji mizigo na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa.

Nguhulla amesema baada ya kutoa ushauri huo baadhi ya watu wamejitokeza wamemshutumu kwa kile alichokifanya na kusema kuwa bado haiwezi kuwa sababu ya kukwamisha mpango wake huo.

“Agosti 26, mwaka huu alitokea mtu kunitukana kwa kutumia moja ya televisheni nchini na kusema mimi nilimwandikia barua kumshauri Rais kuhusu waraka unaoitwa delivery order na tozo zake, lakini siwezi kurudi nyuma kuacha kumshauri Rais Magufuli,” amesema.