Njombe kutumia mifumo ya ukusanyaji kodi

07Feb 2016
Furaha Eliab
Nipashe Jumapili
Njombe kutumia mifumo ya ukusanyaji kodi

HALMASHAURI mkoani Njombe zimetakiwa kutumia mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili kuinua mapato ya ndani ambayo yatatumika kufanya maendeleo ya halmashauri hizo kwa kushirikiana nna serikali.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawara wa mkoa wa Njombe Joseph Makinga wakati akifunga mkutano wa baraza za madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Alisema kuwa haiwezikani halmashauri ikafanya maendeleo kwa kutegemeda fedha kutoka serikali kuu pekee hivyo halmashauri zinatakiwa kuhakikisha kuwa zinakusanya mapato yao ya ndani ili kuhakikisha kuwa fedha zinazo patikana zinasaidiana na zile za serikali kusukuma bajeti.
Makinga alisema halmashauri zihakikishe kuwa zinasimamia kikamilifu vyanzo vyake vya mapato na ili kuona kiwango cha makusanyo yake kinaongezeka kama walivyo jiwekea malengo.
Aliongeza kuwa haiwezekani halmashauri ikafanya maendeleo kwa kutegemea vyanzo vya serikali pekee katika maendeleo na kufanya uzembe katika ukusanyaji wa mapato yake.
Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri hiyo Valentino Hongoli alisema kuwa watendaji wake watawasisitizia kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa kikamilifu ili kupandisha mapato yake maradufu.
"Halmashauri yetu inategemea sana mapato yake kwa ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya miti na viazi, hivyo nitahakikisha mapato yanaongezeka kwa kukusanya kupitia sehemu hizo" alisema Hongoli.
Aliongeza kuwa katika maeneo yote ya halmashauri yake, ni marufuku magari ya mizigo kusafiri usiku kwa kuwa safari za usiku zina saidia kukwepesha kodi, hivyo hairuhusiwi kwa gari yoyote kupita usiku.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alisema kuwa katika halmashauri yake kuna changamoto ya baadhi ya watu wanao kwepa kodi na wengine kulipa pungufu, kitu kinacho sababisha halmashauri kutotimiza malengo yake kwa wakati.
Mwanzinga aliwaomba madiwani kusimamia makusanyo katika kata zao na kutumia mikutano kutoa elimu ya kulipa kodi.

Habari Kubwa