NMB yazindua promosheni mpya ya Pata Patia

25Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
NMB yazindua promosheni mpya ya Pata Patia

BENKI ya NMB imezindua promosheni mpya ijulikanayo kama Pata Patia ambapo zaidi ya Sh. milioni 300 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo.

Kaimu wa shughuli za benki binafsi, Boma Raballa.

Uzinduzi wa promosheni hiyo ilifanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu wa shughuli za benki binafsi, Boma Raballa, alisema promosheni hiyo itawapa wateja wapya wa benki hiyo na waliopo kushindania kitita hicho cha fedha.

Raballa alisema kila mwezi watapatikana washindi 24 watakaokuwa wameweka fedha zao katika akaunti zao za NMB kwenye zaidi ya matawi 170 kote nchini na mawakala mbalimbali nchi nzima.

Alifafanua kuwa kadiri mteja wa benki hiyo atakavyozidi kuweka, ndivyo atakavyojiongezea nafasi zaidi za kushiriki droo na kushinda kila mwezi.

Mwapachu alisema Promosheni hiyo itadumu kwa miezi sita na kwamba washindi watapatikana kwa kuzungusha gurudumu la pesa chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.

Kwa majaribio, waandishi wawili wa jijini Dar es Salaam, walishiriki droo ambapo mmoja alijinyakulia Sh. milioni moja na mwingine Sh. 600,000.

Mwapachu alitoa wito kwa wateja wa benki hiyo na wapya, kushiriki droo hiyo ili washindie fedha hizo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko NMB, Rahma mwapachu, alisema ili kujiunga na promosheni hiyo mtaeja atatakiwa kuweka fedha kwenye moja ya akaunti za muda maalum za benki hiyo, NMB Bonus, NMB Junior, Akaunti Binafsi, Akaunti ya Mwanfaunzi, Akaunti ya Chap Chap, Akaunti ya Biashara, Akaunti ya Biashara ya Kuweka na Pamoja Akaunti.

Mwisho.

Habari Kubwa