Norway yakunwa na Tanzania matumizi fedha za misaada

02Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
korogwe
Nipashe
Norway yakunwa na Tanzania matumizi fedha za misaada

SERIKALI ya Norway imeelezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na serikali
nchini katika kusimamia fedha ilizotoa mwaka 1995 kugharimia miradi
ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme nchini.

 

Akizungumza juzi baada ya kutembelea kituo cha New Pangani Falls,katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili, Waziri waMaendeleo wa Norway, Nicolai Astrup, alisema walitoa fedha hizo kwaserikali kutokana na uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo ikiwamousimamizi mzuri uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Waziri huyo pia alisema serikali yake imeongeza mkataba wakusaidia uwekaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijiji kutokamwaka 2020-2021 baada ya kuridhika na usimamizi mzuri uliofanywakatika ukarabati wa vituo hivyo.

“Nipo hapa Pangani Falls, Norway na Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu.Nimekuja kufuatilia matokeo ya msaada tuliotoa mwaka 1995 kwa vituovya kuzalisha umeme utokanao na vyanzo vya maji,” alisema.

Baadaye akizungumza na wananchi wa mji wa Bagamoyo wilayani Korogwe,Waziri huyo alisema umeme ni muhimu katika maendeleoya wananchi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kwamba serikaliyao itanedelea kushirikiana na Tanzania kusaidia nishati hiyo.

Serikali ya Norway ilitoa dola za Kimarekani dola milioni 126awamu ya kwanza na kisha awamu ya pili ya ukarabati wa vituo vyakuzalisha umeme vya Pangani, Kidatu, Kihansi, Nyumba yaMungu na Mtera uliomalizika Aprili, mwaka huu, walitoa Sh.  bilioni 21.

Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisifu juhudikubwa zinazofanywa na serikali ya Norway kuwekeza kwenye sekta yanishati kwa nchi hatua ambayo imewezesha maeneo mengi kunufaika nahuduma hiyo muhimu.

Licha ya kufanyia ukarabati, pia ilishiriki katika ujenzi kwakutoa zaidi ya asilimia 42 pamoja na serikali ya Sweden kwenye ujenziwa kituo hicho hatua ambayo imesaidia kufanya kazi zake kwaufanisi zaidi.

Alisema serikali ya Norway ni wadau wakubwa kwenye utekelezaji waumeme vijijini na Tanga ni miongoni mwa mikoa iliyopata fursaya uwapo wa vijiji vinavyofadhiliwa na katika mradi wa umeme vijijini.

“Naishukuru sana serikali ya Norway kwajitihada kubwa inazofanya kwa uwekezaji kwenye sekta ya nishatikatika nchi yetu. Si suala la kupeleka umeme vijijini pekee lakiniwamekuwa wakiwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi,” alisema.

 

 

Habari Kubwa