RC akomaa wafugaji kuondoa mifugo kwenye ranchi

13Jan 2021
Grace Mwakalinga
Mbarali
Nipashe
RC akomaa wafugaji kuondoa mifugo kwenye ranchi

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesisitiza kusimamia agizo lake la kuwapa siku sita wafugaji kuondosha mifugo kwenye ranchi za Usangu, mashamba ya Ihefu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Chalamila alitoa agizo la kuwataka wafugaji kuondoka katika ranchi hiyo mwishoni mwa wiki akiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Hivyo, ikiwa kesho ndiyo siku ya mwisho wa agizo hilo, Chalamila amewatahadharisha wafugaji hao kuondoka mapema katika ranchi hizo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Chalamila alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kwa wawekezaji ambao wamekuwa wakilalamika kwamba wafugaji hao wamevamia mashamba yao wakiwa na mifugo ikiwamo ng'ombe na mbuzi.

"Nitasimamia agizo hili kuhakikisha hakuna mifugo yoyote kwenye Hifadhi ya Ruaha na maeneo mengine ya uwekezaji, msihoji ni kwa namna gani nitaondoa ila mtakiona Alhamisi," alisema Chalamila.

Awali Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa Ruaha, Sharif Abdul, alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, kuna wimbi kubwa la wafugaji ambao huingiza mifugo kwenye hifadhi hiyo.

 

Alisema hali hiyo inahatarisha afya na usalama wa wanyamapori katika hifadhi hiyo, pindi wanapoingiliana na mifugo ya wananchi.

Aliongeza wamekaa vikao vya kujadili tatizo hilo mara tatu ikiwajumuisha viongozi wa vijiji pamoja na wafugaji, lakini hakuna suluhisho lolote....soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa