`Sekta ya biashara inakua kwa asilimia 40 kila mwaka'

02Mar 2016
Dar
Nipashe
`Sekta ya biashara inakua kwa asilimia 40 kila mwaka'

SEKTA ya biashara inakua kwa asilimia 40 kila mwaka, huku biashara ndogo na kati (SME’s) zikichukua asilimia 70 ya biashara yote katika uchumi wa ndani unaochagizwa na ukuaji wa sekta ya biashara.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya ysats.com, umebaini vyombo vya habari navyo vimebadilisha mazingira kwa wafanyabiashara wadogo na kwamba sekta zote zimeguswa na biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema mtandao huo pia umebaini ukuaji wa sekta ya biashara inaweza kuchangiwa na maendeleo ya ukuaji wa teknolojia.

Alisema upatikanaji wa intaneti umeongezeka na kwa sasa zaidi ya Watanzania milioni tisa wanapata huduma ya intaneti na kuchangia ukuaji wa sekta ya biashara.

“Wakati viwanda vinaguswa na teknolojia ya mtandao, biashara ya magari ni miongoni mwa biashara iliyokua zaidi kutokana na teknolojia hii. Mtu yeyote anayeweza kuuza magari kwa wauzaji wa kibiashara au binafsi, wanatakiwa kutambua umuhimu wa biashara mtandao na jinsi kujiinua,” alisema.

Ebbersten alisema kuwa ripoti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, inaonyesha kuwa vyombo vya habari vya kidigitali ikiwamo mitandao ya kijamii, vimechangia kuongeza ufanisi wa kuwafikishia bidhaa wateja wanaowataka.

“Biashara mtandao imesaidia kampuni na wauzaji wanaotumia huduma ya masoko mtandao kwa kuweka bidhaa na huduma zao kwa wateja walengwa. Hii ni fursa kwa watoa huduma kutoa taarifa zao kwa idadi kubwa ya wateja,” alisema.

Ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, vyombo vya habari vya digitali imeongeza gharama za ufanisi wa bidhaa katika kujaribu kufikia lengo kuwafikia wateja.

Habari Kubwa