Serikali kuwapatia mafunzo,kipimia udongo maafisa ugani 1,500

11Jun 2021
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Serikali kuwapatia mafunzo,kipimia udongo maafisa ugani 1,500

SERIKALI itawapatia mafunzo Maafisa Ugani 1,500 ikiwemo kuwapatia pikipiki na kifaa cha kupimia Udongo (Soil Kit) ili kuwapa uhakika wakulima aina ya mazao wanayotakiwa kulima katika maeneo husika.

Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe na Mkurugenzi wa maendeleo ya Mazao wa wizara hiyo Nyasebwa Chimago wakimskiliza mtaalamu na mratibu wa mbegu Ikunda Masawe

Aidha Wizara ya Kilimo imesema itarudisha mfumo wa zamani ambapo Afisa Ugani atalazimia kuvaa sare maalum ya kumtambulisha kama ni bwana shamba mbele ya jamii.

Akizungumza jana jijini hapa,katika ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Kilimo, Husein Bashe amesema, watahakikisha mabwana shamba wanarudi shambani lakini wanapewa mafunzo ili waendane na teknolojia ya sasa.

Amesema tayari Wizara ya Kilimo wameandaa Bihawana kama kituo cha kwa ajili ya kuwapa mafunzo ili waendane na teknolojia ya sasa.

Amesema mkakati huo utaanzia katika mikoa ya Dodoma,Singida,Manyara na Simiyu ambayo imepewa kipaumbele katika uzalishaji wa zao la Alizeti.

Amesema maafisa Ugani hao wote hawatatoka katika mikoa hiyo ilioanishwa,wengine watatoka katika mikoa mingine.

Habari Kubwa