Serikali kutekeleza mradi wa kudhibiti sumu kuvu kwa kutoa elimu

05Aug 2022
Renatha Msungu
MBEYA
Nipashe
Serikali kutekeleza mradi wa kudhibiti sumu kuvu kwa kutoa elimu

WIZARA ya Kilimo inatekeleza mradi wa kudhibiti sumu kuvu wenye thamani ya Shilingi bilioni 80 ambao umelenga kuwaelimisha wananchi kuhifadhi chakula katika hali ya usalama ambayo haitaruhusu sumu hiyo kuingia  kwenye mazao.

Merce Buta Mtaalamu wa kilimo,kutoka wizara ya kilimo.

Hayo yamesemwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Kilimo, Mercy Buta katika maonyesho ya wakulima Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja John Mwakangale Jijini Mbeya.

Buta amesema,mradi huo unatekelezwa kwenye mikoa 10 na katika halmashauri 18 ,pia unatekelezwa Zanzibar katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Amesema,lengo la mradi huo ni  kuimarisha usalama wa chakula ndani na nje ya nchi pamoja na afya ya jamii.

“Kwa hiyo tupo katika maonyesho haya hapa Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu sumu kuvu ambayo ni sumu inayosababishwa na kuvu (fangus) .”amesema Buta

Kuhusu madhara ya sumu kuvu Mtaalam huyo amesema,madhara ya sumu kuvu ni halisi na kwamba mtu akila kwa muda mrefu chakula chenye sumu matokeo yake ni kupata kansa.

“Kansa zinazoripotiwa asilimia 30 inaweza kuwa zinasababishwa na sumu kuvu, ndio maana mradi wa kuelimisha jamii umekuja ili  kukabiliana na suala hilo .”amesisitiza

Vile vile amesema,katika kudhibiti sumu kuvu,wizara imekuja na teknolojia mbalimbali zinazoweza kudhibiti sumu kuvu hiyo vikiwemo viuatilifu pamoja na teklojia nyingine katika kuhifadhi mazao tangu wakati wa kilimo mpaka kuhifadhi mazao.

Kwa upande wake mtaalam wa kutoka Wizara ya Kilimo Hilda Shegembe amesema,moja ya teknolojia ni kipukucho mahindi ambayo ni teknlojia rahisi inayoweza kudhibiti sumu kuvu na bei yake ni rahisi . 

Habari Kubwa