Shirika lajitosa ajira kwa vijana

04Mar 2019
Dege Masoli
TANGA
Nipashe
Shirika lajitosa ajira kwa vijana

SHIRIKA la Konrad Adenauer linalofanya kazi chini ya Ujerumani, limepanga kupunguza changamoto mbalimbali ikiwamo kutoa elimu ya uchumi jamii yenye lengo la kuwawezesha Watanzania kujiajiri.

Akizungumza katika kongamano la elimu ya uchumi jamii lililoshirikishawanafunzi wa vyuo mbalimbali jijini Tanga, Ofisa Miradi wa shirikahilo, Mary Tagalile, alisema lengo kuu ni kubadilisha mtazamo katika sekta ya ajira hususan kwa vijana ambao wamekuwa wakilalamika kukosa nafasi serikalini.

Tagalile aliwataka vijana kujitambua na kuachana na dhana ya kutegemea kuajiriwa pindi wanapohitimu masomo na badala yake wawe wabunifu katika kukabiliana na changamoto za ajira kwa kujiajiri kwa kuwa sekta hiyo ndio pana na yenye uwezo wa kuwafikia watu wengi zaidi.

"Shirika limeona ni vyema kutoa elimu kwa vijana kujitambualakini pia kuwapa elimu ambayo itawajenga katika kukabiliana nachangamoto ya ajira, huku lengo likiwa ni kupata maendeleo kupitiasekta binafsi," alisema.

Naye Richard Jackson, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema vijana wengi wanakata tamaa ya maisha kutokana na kukosa ajira, hivyo kupitia kongamano hilo watapata mbinu za kukabiliana na changamoto za ajira.

"Mnajua hakuna mtu ambaye anaweza kuwaletea maendeleo zaidi yaninyi wenyewe, hivyo mnatakiwa kuwa na uthubutu, mfungue masikio yenu na muwe na jicho la kuona namna ambavyo mnaweza kutengeneza misingi bora ya maisha yenu bila kusubiri kuajiriwa," alisema Jackson. 

Wakizungumza baada ya kongamano hilo, baadhi ya wanachuo walisema elimu waliyoipata imewasaidia kutambua tatizo linalofanya kuwapo kwa ongezeko la vijana mitaani kuwa nipamoja na kushindwa kuwa wabunifu na kuahidi kuwa mabalozi wazuri kwawenzao. 

"Tumejua mbinu mbalimbali za kujiajiri, hivyo kupitia elimu hiituliyopewa leo (juzi) tutaweza sasa kufanya uamuzi mzuri wa kujiajiribaada ya kumaliza chuo lakini pia tunaahidi kuwa mabalozi kwa wenzetu ambao hawajapata fursa ya kufika hapa," alisema Musa Mahenge, mwanafunzi kutoka Chuo cha Elimu Sahare.

Habari Kubwa