Stanbic yaipiga jeki shule iliyokumbwa na mafuriko

26Feb 2016
Beatrice Shayo
Dar
Nipashe
Stanbic yaipiga jeki shule iliyokumbwa na mafuriko

BENKI ya Stanbic imesaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Magomeni mkoani Mtwara iliyokumbwa na mafuriko.

Benki ya Stanbic.

Shule hiyo ilijengewa madarasa mawili pamoja na kupatiwa sare za shule 700 vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 50.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Stanbic, Desideria Mwegelo, alisema lengo la kuisaidia shule hiyo ni moja ya mikakati yao katika kuisaidia jamii.

“Hapo awali tuliombwa kuchangia vyakula baada ya mafuriko, tukaona tunaweza kufanya kitu ambacho kitadumu kwa muda mrefu,” alisema.

Alisema mbali na kujenga madarasa, benki hiyo imeweka umeme katika shule hiyo pamoja na kununua madawati.

Habari Kubwa