Standard Chartered yazindua malipo kwa njia ya mtandao

17Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Standard Chartered yazindua malipo kwa njia ya mtandao

BENKI ya Standard Chartered, imezindua mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao ujulikanao kama ‘Straight2Bank-NextGen’, utakaowawezesha wananchi kulipia huduma mbalimbali zikiwamo za serikali.

Akizungumza kuhusu huduma hiyo jana jijini Dodoma, Mtaalamu wa Huduma za Benki Mtandao na Malipo ya Serikali Mtandao, Mwiga Kapya, alisema huduma hiyo itawezesha mtumaji na mpokeaji kupata taarifa ya papo hapo pindi muamala wa malipo unapofanyika.

“Pia, mtumaji wa fedha atapokea stakabadhi ya malipo papo hapo kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu ya malipo yake kwa baadaye,” alisifu.

Alisema huduma hiyo inawarahishia wateja kutokukosea wakati wakifanya malipo yao, akibainisha kuwa mwananchi yeyote anaweza kuitumia.

“Benki ya Standard Chartered inaendelea kuboresha huduma zake za dijitali ili kuwasaidia wananchi na wafanyabishara wakati wakifanya malipo yao hususani malipo ya kodi, tutaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali,” alitamba.

Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Sausi, aliipongeza Benki ya Standard Charted kwa kuanzisha mfumo huo ambao unawahusu wanananchi wote hata wasiotumia huduma za kibenki.

Habari Kubwa