Tanga yapoteza Sh. 50m/- kodi ya uvuvi

19Mar 2016
Lulu George
Tanga
Nipashe
Tanga yapoteza Sh. 50m/- kodi ya uvuvi

SERIKALI Wilaya ya Pangani inapoteza mapato ya zaidi ya Sh. milioni 50, katika kipindi cha Januari mpaka Machi, zinazotokana na kodi ya mazao ya uvuvi.

naibu waziri wa fedha na uchumi, Dk.Ashiatu Kijaji.

Upotevu huo umetokana na wavuvi wa wilaya hiyo kushindwa kulipa leseni za uvuvi, leseni za vyombo vya uvuvi na ushuru wa mazao ya uvuvi tangu kipindi hicho, mwaka huu.

Wilaya hiyo yenye wavuvi wapatao 1741 na vyombo vya uvuvi 380, kila chombo hutozwa Sh. 22,500 na leseni ya uvuvi ni Sh. 22,500, lakini mpaka sasa ni wavuvi 14 tu waliokata leseni na vyombo vitatu tu vilivyokata leseni ya kufanya shughuli hiyo.

Akizungumza na Nipashe, Ofisa Uvuvi wa wilaya, Chitambo Kauta, alisema kwa sasa wanatoa elimu kwa wavuvi ili waweze kulipa leseni kwa hiari yao kabla ya mwezi Machi, mwaka huu, na sheria itaanza kuchukua mkondo wake.

Kwa mujibu wa sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni ya uvuvi ya mwaka 2009, kila mvuvi anatakiwa kukata leseni ya uvuvi na leseni ya chombo cha uvuvi anachofanyia kazi .

Kauta alisema mwisho wa mwezi Machi, mvuvi atakayefanya kazi zake bila leseni, atapaswa kulipa faini ya Sh. 50,000 na tozo la ziada kwa nusu ya fedha anazolipa kwenye leseni.

Habari Kubwa