TBS wapewa changamoto kutembelea maeneo ya uzalishaji

22Jun 2016
John Ngunge
Arusha
Nipashe
TBS wapewa changamoto kutembelea maeneo ya uzalishaji

SHIRIKA la Viwango la Tanzania (TBS) limepewa changamoto kuacha kufanya kazi kwa mazoezi na kukaa ofisini kusubiri kupelekewa taarifa.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko

Alilitaka shirika hilo, kuongeza udhibiti ili kuzuia bidhaa zisizo na viwango zisiingie sokoni.

Alitoa changamoto hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kimaifa la Shirika la Viwango Barani Afrika jijini hapa juzi.

Aliwataka wafanyakazi wa TBS kutembelea viwandani ambako wafanyabiashara wanazalisha bidhaa.

“Tatizo la bidhaa bandia ambazo hazina viwango ni kubwa hivyo shirika hili halina budi kuongeza usimamizi na udhibiti, ambao utawezesha kuzalishwa bidhaa zenye ubora unaotakiwa,” alisema.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko, alisema katika kukabiliana na bidhaa zisizokuwa na viwango, shirika hilo limefungua ofisi ngazi ya kanda katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya, lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi.

“TBS, imeshafungua ofisi kwenye maeneo yote ya mipakani ikiwamo, Namanga, Holili, Sirari, Kasumulo, Kabanga, Tunduma, Rusumo, na Mtukula,” alisema.

Alisema shirika hilo limefungua ofisi hizo kutokana na changamoto iliyopo ya uuingizwaji wa bidhaa toka nje ambazo hazina viwango na hatari kwa mlaji.

Alisema shirika hilo lipo kwa ajili ya kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa bora zenye viwango na kudhibiti bidhaa zisizo na viwango zikiwemo za ndani na nje.

Habari Kubwa