Tembo wawafanyia vurugu wakulima Bunda

19Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Bunda
Nipashe
Tembo wawafanyia vurugu wakulima Bunda

MAKUNDI ya tembo kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, yamevamia mashamba ya wakulima na kushambulia mazao kijiji cha Kunzugu, wilayani Bunda, mkoani Mara.

tembo.

Diwani wa Kata ya Kunzugu, Pasaka Samson, alisema tembo hao walivamia mashamba na kushambulia mazao ya wakulima yakiwamo ya mpunga uliokuwa tayari kwa kuvunwa.

Alisema tembo hao hutembea makundi kati ya 20 hadi 60, wamekuwa wakitoka katika hifadhi hiyo nyakati za usiku na kuingia pia kwenye makazi ya watu.

Hata hivyo, alisema amewasiliana na uongozi wa Halmashauri ya mji wa Bunda kupitia kitengo cha wanyamapori, ili waweze kuendesha doria kwa ajili ya kuzuia wanyama hao na zoezi hilo linatarajiwa kuanza leo.

Habari Kubwa