TRA yaendelea kukusanya kodi kwa mafanikio makubwa

03Apr 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
TRA yaendelea kukusanya kodi kwa mafanikio makubwa

​​​​​​​MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika kipindi cha robo tatu yaani mwezi July 2021 hadi March 2022 kwa mwaka wa fedha 2021/22 imekusanya shilingi Trilioni 16.69 ikiwa ni sawa na ufanisi wa 97.3% ya lengo la kukusanya shilingi Trilioni 17.15,-

-makusanyo haya ni ongezeko la shilingi Trilioni 3.1 ukilinganisha na kiwango cha makusanyo cha shilingi Trilioni 13.59 kilichokusanywa kwa kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2020/21 "Ongezeko hili ni ukuaji wa makusanyo ya kodi wa 22.8%" 

Aidha, kwa mwezi Machi 2022, TRA imekusanya shilingi Trilioni 2.06 kati ya lengo la kukusanya shilingi Trilioni 1.98, makusanyo haya ni sawa na ufanisi wa 103.6% na ukuaji wa 23.17% ikilinganishwa na mwezi Machi 2021 ambapo makusanyo yalikuwa shilingi Trilioni 1.67.

"Ifahamike kuwa, makusanyo haya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na: kuongezeka kwa uhiari wa kulipa kodi; kuimarika kwa mahusiano baina ya TRA na walipakodi kunakochagizwa na utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama pamoja na kushughulikia malalamiko ya walipakodi kwa wakati, pia ufanisi huo umetokana na kuimarika kwa uzalishaji wa viwanda vya ndani na biashara za kimataifa"

"TRA inapenda kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa walipakodi wote na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa dhati katika kuendelea kulipa kodi kwa hiari, kipeke tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia kwa miongozo na msaada wake katika kutekeleza wajibu wetu, ulipaji kodi sahihi wa hiari na kwa wakati kumeifanya TRA ivuke lengo mwezi Machi 2022 na kunaiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama vile kugharamia miradi ya maendeleo, kutoa huduma za kijamii, ulinzi na usalama wa nchi"

Habari Kubwa