TRA yavuka lengo la ukusanyaji

06Dec 2017
Mary Mosha
Nipashe
TRA yavuka lengo la ukusanyaji

MAMLAKA ya Mapato (TRA), katika wilaya za Hai na Siha,imevuka lengo la makusanyo ya kodi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 ambayo ilianza mwezi Julai hadi Septemba 30,mwaka huu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo

Malengo ya ukusanyaji wa mapato katika wilaya hizo kwa kipindi cha robo ya kwanza ilikuwa Sh. 637,120,000, lakini imekusanya Sh. 773,338,418.

Akizungumza katika kikao cha washauri wa kodi katika Wilaya ya Hai na Siha, Meneja wa TRA, Specioza Owure, alisema wamevuka malengo waliojiwekea kutoka na elimu kwa wananchi kuhusu ulipaji wa kodi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu, alisema mpaka sasa wamebaini maeneo yanayopaswa kulipa kodi ili kuondokana na udanganyifu na ukwepaji wa kodi.

Mchomvu alisema wameandaa kanzi data kuanzia ngazi za vijiji hadi wilaya ambazo itasaidia kutambua vyanzo vyamapato na kurahisisha ufuatilia ulipaji wa kodi hali itayaosaidia kuendelea kukusanya mapato yote kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Siha, anaye kaimu ukuu wa wilaya ya  Hai, Onesmo Bawelu, alisema serikali imeridhika na hali ya ukusanyaji wa mapato unaofanywa na TRA  katika wilaya hizo.

Alisema bado wanakabiliwa na changamotoya baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kutoa risiti.Aliwataka wanasiasa kuacha kupotoshawananchi kuwa mapato ya nchi yameshuka na badala yake wachukue taarifa za ukusanyaji mapato kutoka mamlaka husika na kueleza wananchi.

“Natambua kuwa wabunge wote ni wajumbe wa kamati za ushauri juu ya kodi katika wilaya wanazotoka ni vyema kuelimisha wananchi hali ya ukusanyaji wa mapato ya nchini na kuacha kueneza habari kwenye mitandano ya kijamii kuwa mapato ya nchi yameshuka.” 

Habari Kubwa