Ummy akabidhi hundi ya milioni 300 mkopo kwa vikundi 37 Tanga

26Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
TANGA
Nipashe
Ummy akabidhi hundi ya milioni 300 mkopo kwa vikundi 37 Tanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu amekabidhi hundi ya Sh.milioni 300 kwa vikundi 37 vya Jiji la  Tanga ikiwa ni mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Fedha hizo ni mapato yake ya ndani  kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2020/21.Waziri Ummy amekabidhi hundi hiyo mapema leo Aprili 26,2021 katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Jiji la Tanga.

"Ni furaha kwangu kuona Jiji mmetimiza wajibu wenu sasa nivitake vikundi ambavyo mmapokea fedha hizi mkazifanyie kazi na kuzirejesha kwa wakati ili wenzenu wengine waweze kunufaika na mikopo hii ya Serikali,"amesema

Naye,Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Maeji amesema kwa Bajeti ya Jiji la Tanga walipanga kutoa Mikopo ya asilimia 10 yenye jumla  ya shilingi Bil. 1.2 na mpaka sasa wameshatoa sh. Mil 994 sawa na asilimia  81 ya malengo waliyojiwekea.

Habari Kubwa