Vijana wapewa siri

26Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Vijana wapewa siri

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa juzi aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na taifa.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, Majaliwa aliwasihi wakazi wa mipakani kuweka kipaumbele katika ulinzi wa mipaka hiyo ili kuimarisha amani na utulivu nchini.

Waziri Mkuu alisema hayo wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Nachingwea.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili zilizoisha jana, alisema ili vijana wapate maendeleo ni lazima wafanye kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu huyo alikagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.

Alisema Serikali imetoa Sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi za wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.

Habari Kubwa