Vijana waziona, wazitumia fursa

18Mar 2019
Nebart Msokwa
MBEYA
Nipashe
Vijana waziona, wazitumia fursa

VIJANA 85 wa kata sita za Jiji la Mbeya wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali ikiwamo kutengeneza bidhaa mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi, kujiajiri na kuepuka utegemezi.

Mafunzo hayo yalitolewa na mashirika ya kiraia ya Shop na The Foundation for Civil Society katika kata za Iyela, Isyesye, Ilemi, Ilomba, Maanga na Ruanda ambapo vijana hao waliunganishwa kwenye vikundi.

Katibu wa Shop, Olais Oleseenga, alisema ili kutekeleza mradi huo walipewa ruzuku ya shilingi milioni 30 kuwapatia elimu vijana wa kata sita jijini hili.

Alisema lengo la mradi huo ni kuhakikisha vijana wanakuwa kiuchumi na kuimarika kwa kufanya ujasiriamali ambao utakuwa na manufaa kwao, vikundi mbalimbali na taifa.

Alisema awali shirika hilo lilitoa elimu kwa vijana juu ya kuzitambua fursa mbalimbali zinazowazunguka ndani ya kata zao na kutambua sera ya vijana ya 2007 na baadaye wakaanza kutoa elimu ya ujasiriamali.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Mbeya, Onna Geofrey, alisema kwa sasa vijana wanatakiwa kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kupitia mifuko ya vijana.

Habari Kubwa