Katibu wea soko hilo, Furahisha Kambi, alisema juzi kuwa kitendo cha wafanyabiashara hao kufanya biashara nje ya soko, kinasababisha wateja kuishia nje hivyo kuwafanya wanaofanya kazi zao kihalali na kulipa ushuru kutopata wateja.
“Malalamiko yanakuwa mengi kwa wafanyabiashara walioko ndani, kutopata wateja kutokana na wengi kuishia nje,” alisema.
Aliongeza kuwa wameshalalamikia katika uongozi wa Mansipaa ambao ndio una uwezo wa kuwatoa sokoni wafanyabiashara hao kutokana na kuchukuwa ushuru, lakini mpaka sasa hawajaondolewa.
Alisema kutokana na kushindwa kuwaondoa, wanatarajia kuchukua hatua za kisheria ikiwamo kwenda mahakamani ili wasaidiwe.
Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, alisema haba taarifa na suala la wafanyabiashara kufanya biashara nje ya soko na kwamba atalifuatilia.
"Mgambo wapo katika soko kwa ajili ya kusimamia watu wasifanye biashara nje. Kama unasema biashara ziko nje zinaendelea kufanywa nitafuatilia kwa wale wanaosimamia na kisha nitakujulisha,” alisema.
mwisho