Wachina watangaza neema kwa wakulima wa mhugo

08Feb 2016
Idda Mushi
Nipashe
Wachina watangaza neema kwa wakulima wa mhugo

FURSA ya biashara ya zao la mhogo imezidi kukukua kwa wawekezaji kutoka nchini China, kutaka kununua tani milioni mbili za mhogo mkavu.

Aidha, Wachina hao wameahidi kuendelea kuongeza nusu zaidi ya kiasi hicho kila mwaka iwapo wataridhishwa na upatikanaji wa uhakika wa mhogo ulio bora. Mratibu wa zao la Mhogo kitaifa, Dk. Geofrey Mkamilo, alisema ujio wa Wachina hao, ni fursa kwa wakulima kuhakikisha wanalima mbegu bora zilizofanyiwa utafiti, ambazo zina uwezo wa kuzaa tani 20 hadi 30 ya mhogo kwa hekta. Alisema uwezo wa mbegu za kienyeji ni mdogo na hazihimili magonjwa sugu ukiwamo wa michirizi ya kahawia na bato bato kali. “Mhogo kwa sasa siyo zao la kinga ya njaa pekee bali ni zao la biashara, wakulima hawana budi kutumia fursa zilizopo kuhakikisha wanatumia mbegu bora na kuzalisha mhogo kwa wingi ili kujikwamua na umaskini,” alisisitiza Dk. Mkamilo. Ofisa kilimo msaidizi kutoka kituo cha utafiti na maendeleo cha Naliendele, Julius Chacha, alisema katika shamba hilo wanakusudia kupanda mbegu zaidi ambazo hazishambuliwi na magonjwa ambazo watazisambaza kwa wakulima.

Habari Kubwa