Wafanyabiashara watakiwa kutumia teknolojia katika shughuli zao

20Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wafanyabiashara watakiwa kutumia teknolojia katika shughuli zao

JAMII ya wafanyabiashara mjini Mwanza imehamasishwa kutumia teknolojia na ubunifu katika kuendesha shughuli zao ili kutatua changamoto zinazowakabili.

waziri wa viwanda, charles mwijage.

Wito huo ulitolewa na mjini hapa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Ubunifu, Ujasiriamali na Ushindani wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dugushilu Mafunda.

Alisema utumiaji wa teknolojia ya kisasa utawajengea uelewa vijana na kuwa wabunifu na wajasiriamali wazuri.

"Yapo mambo mengi yanayosababisha teknolojia isiingie sokoni, moja ni ukosefu wa masoko, viwango, ubora na sera mbovu, lakini pia ushindani katika uanzishwaji biashara kupitia Tehama na ni ngumu sana mfumo wa ubunifu kuweza kupata mkopo,” alisema.

Mkurugenzi na mwanzilishi wa mifumo mbalimbali inayotumia kompyuta, Godfrey Magilla, alisema alianzisha kampuni ya kutengeneza softiwea ndogondogo na kuziingiza sokoni mwaka 2012 na kwa sasa amefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 14.

"Changamoto tunayo kutananayo ni utayari wa wateja kuchukua softiwea tunazotengeneza kupitia teknolojia ya Tehama, lakini huwa tunatoa elimu, kila mwaka tunatenga miezi miwili ya kufundisha programu za softiwea,’’ alisema.

Alisema kampuni hiyo imekuwa ikifakanya kazi na mitandao mbalimbali ya simu kama Tigo na Airtel kwa kufungua mifumo inayotumiwa na wateja wake kama Tigobackup, Airtelbando, vifurushi na matumizi ya intaneti kupitia simu ya mkononi.

"Tumethubutu kutengeneza programu nyingi na kuziingiza sokoni na katika hili tumekuwa tukishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia, siyo jambo gumu mtu yoyote anaweza kuthubutu hususan wajasiriamali," alisema Magila.

Habari Kubwa