Waiomba Manispaa Ilala kuwajengea vyoo

26Feb 2016
Yasmine Protace
Dar
Nipashe
Waiomba Manispaa Ilala kuwajengea vyoo

WAFANYABIASHARA katika soko la Kiwalani Kigilagila, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, wameiomba manispaa hiyo kuwajengea vyoo ili waachane na tabia ya kuchangia choo kimoja na wanaume.

Wamesema katika soko hilo lenye zaidi ya wafanyabiashara 70, wanalipa ushuru wa Sh. 200 kila siku, lakini choo kilichopo hakina ubora.

Mathalani, wamesema milango ya vyoo vilivyopo humfanya mtumiaji akiwa ndani kuonekana na watu wanaopita jirani na eneo hilo.

Wafanyabiashara hao walisema matundu mawili ya vyoo yaliyopo hutumiwa na wanaume na wanawake.

"Hapa kama unavyoona, matundu ya choo ni mawili, hakuna kusema hiki ni cha wanaume au wanawake, tunajikuta wote tunaingia humo humo, na zaidi havina ubora," alisema mmoja wa wafanyabiashara hao, Nasra Selemani.

Msemaji wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, alithitisha soko hilo kukabiliwa na changamoto ya choo.

"Choo kweli hakijitoshelezi, afisa afya na afisa masoko, wanafuatilia jinsi ya kutatua changamoto za choo katika soko hilo,''alisema.

Aliongeza kuwa, kunampango ambao unandaliwa kama soko hilo litabahatika kuingia katika mpango huo, wanaweza kusaidiwa katika kutatua matatizo ya choo.

Habari Kubwa