Wakulima korosho wapewa motisha

07Apr 2017
Stephen Chidiye
Tunduru
Nipashe
Wakulima korosho wapewa motisha

WAKATI wakulima wa korosho wakianza maandalizi ya kupalilia mikorosho, Chama cha Ushirika cha msingi
Mumsasichema Amco’s Ltd  katika kata ya Muhuwesi wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma, kimetoa mifuko 150 ya dawa aina ya Sulphur Duts ya Sh. 5,250,000  kwa wakulima 70 kwa ajili ya kupulizia mikorosho.

Sambamba na motisha huo, pia chama hicho kiliwakabidhi vyeti kutokana na kamilisha kulipia hisa 10 zenye thamani ya Sh. 200,000 kwa kila pamoja na kadi ikiwa ni kuwatambua rasmi kuwa ni wanachama hai.

Walikabidhiwa zawadi hizo katika mkutano mkuu wa kujadili taarifa za maendeleo ya chama hicho kwa 2016/2017.

Mwenyekiti wa chama hicho Issa Kambutu, alisema chama chake kimefanya hivyo kwa lengo la kuongeza hamasa ya kuwafanya waongeze juhudi za uzalishaji wa zao hilo.

Habari Kubwa