Waliodai kugundua dhahabu wagoma kuhama

10Dec 2016
Renatus Masuguliko
GEITA
Nipashe
Waliodai kugundua dhahabu wagoma kuhama

ZAIDI ya watu 1,000 wamevumbua dhahabu katika mtaa wa Nyanza, zaidi ya kilomita tatu kutoka mjini Geita na wameadhimisha miaka 55 ya Uhuru kwa kuapa kutoondoka katika eneo hilo.

Badala yake, wananchi hao wameiomba serkali kuwapatia leseni ya uchimbaji madini hayo kupitia chama cha akiba cha kuweka na kukopa (Saccos) ya Ikumbayaga.

Baadhi ya wananchi hao, akiwamo Juma Kyoma, mmilikiwa wa shamba kulimogunduliwa dhahabu, alisema kwa miaka 20 toka mwaka 1996 aanze kuishi hapa, hajawahi kujitokeza mtu yeyote anayedai kumiliki eneo hilo na kudai na leseni ya uchimbaji madini.

Hata hivyo, alisema baada ya kugundua kuwapo ugunduzi wa dhahabu miezi miwili iliyopita, kuna watu wameanza kujitokea huku wakidai ni wamaliki halali wa eneo hilo na wana leseni ya uchimbaji madini, hivyo kuwataka waondoke.

Pamoja na madai hayo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali (mstaafu) Elias Kyunga, wamewakingia kifua wananchi hao na kusema watahakikisha hawaondolewi.

Naye Makamu Mwenyekitiwa Kamati ya inayosimamia machimbo hayo kwa muda wakati michakato mingine ikiendelea, Peter Chipaka, anasema mchakato umeanza huku wakitaka wananchi walioshiriki ugunduzi huo kupitia Saccos yao ya Ikumbayaga wapewe leseni kumilikishwa machimbo hayo.

Hata hivyo, Chipaka aliilalamikia Ofisi ya Madini Mkoa kwa kutotoa ushirikiano na kuweka mazingira aliyodai yanalenga kuhujumu maombi yao kwa kuwa sera ya sasa ya madini inatoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo kupewa leseni kupitia Saccos na ndicho waanachokifanya kwa kushirikiana na mwenye shamba.

Ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Fabian Mshai, alikiri kuwapo zaidi ya watu 3,000 kunufaika na uwepo na ugunduzi wa dhahabu na kuahidi serkali inayo taarifa rasmi.

Habari Kubwa