Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 29, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkuu wa Huduma za Fedha (MFS), Angelica Pesha, amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa njia mpya na salama ya malipo kwa wateja pale wanapotaka kufanya malipo katika maduka na maeneo mbalimbali ya kibiashara yanayoruhusu mfumo wa Mastercard QR.
"Katika uzinduzi huu tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa huduma yetu ya Masterpass QR kuanzia leo itatambulika kama Tigo Pesa Mastercard QR na hii tumebadilisha jina tu, na napenda kuwahakikishia kwamba hii huduma haijabadilika na itaendelea kuwa vile vile na mtaendelea kupata na kulipa malipo yenu kwa kupitia Tigo Pesa Mastercard QR.," amesema Pesha
Amesema kuwa lengo kuu la kufanya maboresho hayo sambamba na kuja na kampeni hiyo inayowajali wateja, ni kuhakikisha inawapa wateja huduma inayowasaidia kufanya malipo kuwa rahisi zaidi na kama kampuni ya kidigitali siku zote inalenga kutoa sulushisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi.
Amesema kuwa kuanzia leo 29,2019 mtu yoyote atakayefanya miamala ya malipo watapa zawadi ya kurudishiwa fedha hadi asilimia 3 ya fedha kulingana na malipo mtu aliyofanya.
Ameongeza kuwa kumekuwa na uhitaji wa muda mrefu kwa wateja inayowasaidia wateja kufanya malipo kwa njia rahisi na salama na ya haraka hivyo kama Tigo imeona ni vyema kuleta huduma hiyo ya Tigo Pesa Mastercard QR.
“Tigo Pesa Mastercard QR ni fursa ya kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwasababu Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha.Kwa kupitia Tigo Pesa Mastercard QR si tu tunapanua wigo wa utoaji wa huduma zenye usalama kwa wateja bali tunasogeza huduma zenye uharaka karibu na wateja wetu,” amesema Pesha.
Naye Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla amesema Mastercard imejizatiti katika kutafuta njia mbadala ya kifedha kwa kuja na suluhisho linatoa nafasi kwa wateja kupata huduma za malipo zenye usalama na za uhakika.
“Kwa sasa biashara nyingi zinapokea malipo ya Mastercard QR ambapo wateja wanaweza kutumia njia hii ya kidigitali kujipatia zawadi ya fedha kwa malipo waliyofanya.," amesema
Mteja wa Tigo anaweza kufanya malipo kwa njia ya Mastecard QR kupitia App ya Tigo Pesa kwa kuscani QR code au kwa kufuata hatua zifuatazo:
Piga *150*01#,
Chagua namba 5,
Chagua 2, (Lipa kwa Mastercard QR).
Mastercard QR ni njia ya haraka na ya kidigitali yakufanya malipo ambayo kwa sasa inakubalika katika maeneo mbalimbali ya kibiashara kwa wateja wote wa Tigo Pesa.
Mteja anaweza kufurahia huduma ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maeneo maarufu kama vituo vya mafuta vya Puma, migahawa ya KFC, Pizza Hut na Samaki Samaki, Century Cinemax, Supermarket ya Shoppers, JD Phamacies pamoja na maduka ya GSM Mall.