Wateja mafuta wapewa neno

20Nov 2019
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Wateja mafuta wapewa neno

KAMPUNI ya mafuta ya Total imewashukuru Watanzania kwa kuiamini kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zake.

Aidha, imeahidi kuendelea kuwapatia Watanzania huduma na bidhaa zenye ubora.

Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Total Tanzania, Jean-Francois Schoepp, katika hafla ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa wateja, jijini Dar es Salaam.

Schoepp aliwashukuru wateja wao nchi nzima kwa miaka 50 ya uwapo wake nchini. “Hili limewezekana kwa sababu ya uwapo wenu na imani yenu kwenye bidhaa na huduma zetu. Tunawathamini sana, tupo tayari kusikiliza changamoto na mahitaji yenu ili tuweze kuwapatia huduma na bidhaa zilizo bora.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa wa kampuni hiyo, Marsha Msuya, alisema, aliwaahidi a wateja wake kuwa wataboresha huduma zao kulingana na matakwa ya wateja.

Katika sherehe hiyo, Total pia iliwatunukia vyeti na zawadi mbalimbali wafanyakazi wake walioshiriki kwenye mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa na kampuni hiyo.

Habari Kubwa