Wauza dagaa wawagomea ushuru

06Jan 2019
Steven William
PANGANI
Nipashe Jumapili
Wauza dagaa wawagomea ushuru

WAFANYABIASHA kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao hununua dagaa katika ufukwe wa bahari ya Hindi Pangani mkoani Tanga, wamegoma kununua bidhaa hiyo kutokana na kupandishiwa ushuru.

WAKONGO WANAOFANYA BIASHARA YA KUUZA DAGAA KATIKA BAHARI YA HINDI WAMEWEKA MGOMOB BAADA YA KUPANDISHIWA USHURU

Kutokana na hatua ya wafanyabiashara hao kugoma, baadhi ya wauzaji wa bidhaa hiyo wamekosa soko na matokeo yake dagaa wao wameanza kuharibika.

 

Akizungumza juzi katika kikao cha wafanyabiashara katika wilaya ya Pangani,Swaiba Ally alisema wananunua dagaa kutoka kwa wavuvi baharini na wao wanawauzia wafanyabiashara kutoka  Congo.

Ally alisema kila siku wafanyabiashra hao walikuwa wananunuaa dagaa gunia moja na kulipa Sh. 20,000 kwa ajili ya ushuru kwa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani lakini hivi sasa wamegoma baada ya kupandishiwa hadi Sh. 330,000.

 

Alisema wafanyabiashara hao wananunua gunia moja la dagaa kwa Sh. 290,000 kutoka kwa wafanyabiashara wa Pangani, sasa itakuwaje hao walipe ushuru wa Sh. 330,000.

Ally alisema kutokana na kupanda kwa ushuru huo, wafanyabiashara hao wamegoma kununua dagaa, kusababisha dagaa hao kukosa soko kwa kuwa walikuwa wanawategemea Wacongo hao.

 

Kutokana na hali hiyo, alisema wamemwita ofisa uvuvi wa wilaya ili atoe ufafanuzi kuhusu kupanda kwa ushuru na kuwaeleza kuwa amepokea taarifa hiyo kutoka ofisi za uvuvi mkoa.

 

Ally alisema walikuwa wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kuuza dagaa kwa wafanyabiashara hao ambao sasa wamegoma hali ambayo imesababisha maisha yao kuwa magumu.

 

Pia alisema hata wavuvi ambao sehemu kubwa ni kutoka kisiwani Pemba, wameacha kazi hiyo na kurejea kwao.

 

Habari Kubwa