Wavuvi Kanda ya Ziwa kunufaika na ujio wa d.light

20Apr 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Wavuvi Kanda ya Ziwa kunufaika na ujio wa d.light

DIWANI wa Nyamagana, Bhiko Kotecha, amesema wananchi hasa wavuvi watarajia kunufaika na huduma za d.light na kuacha kutumia taa za mafuta baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Kotecha, amesema ni wakati wa d.light kwenda kwenye mialo na kutoa elimu kwa wavuvi ili waachane na uvuvi wa kutumia taa za mafuta  bali watumie d.light ili kuboresha mazingira na kuondokana  na gharama kubwa wanazozitumia kwa sasa.

"Uwepo wa tawi hilo litawasaidia kufika kwa ukaribu nimeona bidhaa zenu ni nzuri na mpangilio wa uuzaji wenu ni mkakati mzuri kwa jamii ya hali zote hakika mnaleta mwanga na kuboresha maisha ya watanzania na hii ndio chachu ya maendeleo" amesema Kotecha 

Saitoti Naikara ni Meneja Biashara d.light, Kanda ya Ziwa, amesema mikakati ya kampuni hiyo ni kuhakikisha ifikapo 2030 wawe wamewafikia wateja zaidi ya Billion 1 ambao watakuwa wanatumia bidhaa zao hiyo inatokana na upatikanaji wake kuwa rahisi na zenye gharama nafuu zaidi na inampa mteja uhuru wa kuchagua kulipa kidogokidogo ana kununua kwa pesa taslimu.

Amesema malengo yao ni kuifikia jamii yote hasa maeneo ya vijijini ambayo yanakabiliwa na changamoto ya nishati mbadala ya uhakika pia wametoa ajira kwa vijana ambao ni mawakala sehemu mbalimbali lakini pia watawafikia wavuvi kwa sababu wana vifaa vinavyokaa na mwanga muda mrefu huku vikiang'aza zaidi ikiwa ni kuonyesha nia thabiti ya kuisadia serikali katika kupambana na uharibifu wa mazingira kuacha kutumia nishati ya mafuta kipindi cha uvuvi 

Kwa upande wake Charles Budeba mmoja wa wateja wa d.light, amesema anajivunia kuwa mteja wa kampuni hiyo kwani wanahuduma nzuri  familia yake inanufaika watoto wamepata mwanga wa kusoma pia mfugo yake kutoshambuliwa na wanyama kama ilivyokuwa mwanzo  kwa sababu ya giza .

Habari Kubwa