‘Muziki gani’ ni dhahabu-Nay

06Feb 2016
Nipashe
‘Muziki gani’ ni dhahabu-Nay

KWELI ya kale ni dhahabu! Rapa Nay wa Mitego anakikumbuka kibao cha ‘Muziki gani’ na kueleza ndio umempatia umaarufu na mafanikio aliyokuwa nayo sasa.

Alisema kibao hicho alichomshirikisha Diamond Platnumz, ulimfungulia njia ya kupata fedha na kujulikana na watanzania.
Pamoja na umaarufu huo, alijikuta akiingia katika wakati mgumu kutokana na umaarufu huo wa ghafla.
“Biashara yangu ilianza pale, niliingiza kipato ambacho sijawahi kukifkiria kwamba kuna siku naweza kuingiza , sawa nilikuwa na vijihela, lakini iliongezeka maradufu,” alisema Nay.

Habari Kubwa