‘Mwaka ulikuwa mgumu, lakini tumefanikiwa...’

23Dec 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
‘Mwaka ulikuwa mgumu, lakini tumefanikiwa...’

Uongozi wa The Guardian Ltd unatoa shukrani zake za dhati kwa wafanyikazi wake wote, hususan timu ya mauzo, kwa kazi kubwa waliofanya mwaka huu.

Timu ya Mauzo ya The Guardian Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja katika hafla ya kufunga mwaka iliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto mstari wa kati ni Meneja wa Fedha Samuel Orgeness na katikati ni Mkurugenzi wa Biashara Ajay Goyal (shati la blue)

Akizungumza baada ya hafla ya pongezi kwa timu hio ya mauzo, Mkurugenzi Wa Biashara wa The Guardian Ltd bwana Ajay Goyal alitoa shukrani na pongezi kwa timu hiyo huku akisema wamefanya kazi ya kujituma na kuwataka waendele na moyo huo huo.

“Huu ulikuwa mwaka mgumu kibiashara, hususan sababu ya mlipuko wa Covid-19,” alisema.

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kazi kubwa iliofanywa na timu ya mauzo kwasababu walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu, tuna wapongeza na tunawashukuru sana,” aliongezea.

Akizungumza kwenye halfa hio hio, Menaja Masoko, Angel Navuri alisema Timu ya Masoko ya The Guardian Ltd imefanyakazi kwa kujituma na kwa weledi mkubwa mno. Alisema ingawa biashara ilikuwa ngumu mwaka huu, timu hio iliendelea kujituma kutimiza wajibu wake.

“Ni washukuru tu wafanyikazi wnezangu kwa kazi kubwa waliofanya na kwa moyo wa ushirikinao walionyesha mwaka mzima,” alisema.

Soma habari zaidi na matokeo mbali mbali hapa: https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa