Amber, Khalifa yametimia tena

08Feb 2016
Nipashe
Amber, Khalifa yametimia tena

KIMWANA Amber Rose na mpenzi wake wa zamani, Rapa Wiz Khalifa wameamua kukubali yaishe na sasa wako pamoja kama marafiki wa karibu na siyo wapenzi.

Wawili hao wamekuwa kwenye vita ya muda mrefu kumgombea mtoto tangu walipotengana, lakini sasa upepo umevuma upande wa furaha.
Kubwa lililowashawishi wapenzi hao wa zamani kuzika tofauti zao ni baada ya kugundua kuwa, kuendelea kulumbana kutamletea matatizo mtoto wao.
Hii ni mara ya kwanza kwa Amber, mpenzi wa zamani wa Kanye West Khalifa kuzungumzia urejeo wa uhusiano wao katika hatua nyingine.
Habari kutoka ndani wa wawili hao, zilidai kuwa baada ya kukaa na kuzungumza, wameamua kuzika tofauti zao ili kuokoa nafasi ya makuzi bora ya mtoto wao.
Pamoja na kuachana, lakini mara kadhaa Amber amekuwa akitamka waziwazi kuwa analikumbuka penzi la Khalifa na anaamini siku moja watakuwa pamoja tena.
Mzozo ulikuwa mkubwa zaidi baada ya West kuzungumzia suala la mtoto wa wawili hao, jambo lililomfanya Khalifa kumjibu vikali msanii mwenzake huyo.

Habari Kubwa